Jumapili 31 Mei 2026 - 20:20
Serikali ya Bahrain imeingia katika vita vya wazi dhidi ya Mashia

Hawza/ Kuharibiwa kwa utambulisho halisi wa Kishia nchini Bahrain si tuhuma inayotolewa dhidi ya mfumo tawala, bali ni mradi hatari ambao unaendelea kutekelezwa bila kuchelewa.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, kwa kunukuu kutoka “Mir’at Al-Bahrain”: Kuharibiwa  utambulisho halisi wa Kishia nchini Bahrain si tuhuma inayotolewa dhidi ya mfumo tawala, bali ni mradi hatari ambao unaendelea kutekelezwa bila kuchelewa, huu ni ukweli ambao watoto wa dhehebu hili wanaendelea kuupitia kutokana na hatua zinazofuatana na za haraka sana zinazochukuliwa kila siku na mamlaka tawala.

Suala hili halina tena nafasi ya shaka, na kujaribu kukanusha mradi huu kwa kurudia kauli zilezile kwamba serikali imefanya “ufunguzi, kuishi pamoja na wengine, na demokrasia” kuwa misingi ya sera zake za ndani, kumekuwa maonesho yaliyoshindwa ambayo hayafikii malengo yake.

Katika hatua za hivi karibuni ambazo zilifanywa moja kwa moja na Hamad bin Isa, mabaraza ya wakfu wa Kisunni na Jaafari pamoja na idara zake yalifutwa, na badala yake kuundwa baraza jipya la wakfu chini ya uongozi wa Waziri.

Hatua hii haiwezi kutenganishwa na mlolongo wa maamuzi ambao hivi karibuni yamelenga dhehebu hili na masuala yake; ikiwa ni pamoja na kuwazingira watu wake, kuwatuhumu kwa uhaini na kuwavunjia heshima, kuwanyang’anya uraia, kuwafuatilia kwa misingi ya itikadi yao ya kidini, kuwafunga wanazuoni wao mashuhuri, na kuwanyima haki ya kutekeleza ibada na alama za dini ambazo zimekuwepo nchini Bahrain kwa miongo mingi.

Pengine jambo hatari zaidi katika uamuzi huu si upande wake wa kiutawala au wa kimfumo, kama serikali inavyojaribu kuuelezea, bali ni alama yake yenye maana ya kina ya kisiasa na kidini.

Wakati usimamizi wa wakfu wa Jaafari unapoondolewa kutoka mazingira yake ya kawaida na kuwekwa chini ya udhibiti wa moja kwa moja wa serikali na Waziri anayehusishwa na mamlaka ya utendaji, ujumbe unakuwa wazi: “Hakuna uhuru kwa jambo lolote la Kishia, hata katika masuala yenye uhusiano mkubwa zaidi na itikadi na upekee wa kidini, hata kama wakfu huo unawakilisha maslahi ya serikali na unaenda sambamba na sera zake.”

Mabadiliko haya hayawezi kufasiriwa isipokuwa katika mfumo wa mradi wa pamoja unaolenga kuijenga upya Bahrain kwa mujibu wa mfumo maalumu wa kisiasa na wa kimadhehebu; mfumo ambao ndani yake dhehebu la Kishia linakuwa kundi linalosimamiwa na kuzingirwa tu, na si mshirika halisi katika taifa.

Suala hili sasa halibaki kuwa tu vikwazo vya kiusalama au hotuba za uchochezi katika vyombo rasmi na nusu rasmi vya habari, bali limevuka hapo na kufikia hatua ya kujaribu kusambaratisha kabisa masuala ya wakfu wa Kishia na kuyafanya kuwa chini ya matakwa ya mamlaka tawala.

Kwa miaka mingi, Mashia wa Bahrain wamekuwa wakiishi chini ya mashinikizo ya kudumu; wakitoa maoni yao hutuhumiwa kwa uhaini; wakishikamana na itikadi na ibada zao huwekwa chini ya uangalizi; na wakidai haki zao za kiraia na kisiasa huwa walengwa wa kufuatiliwa na kuchafuliwa majina yao.

Leo, kulengwa kwa wakfu kunathibitisha kwamba; mradi huu umeingia katika hatua iliyo wazi zaidi, ambayo anuani yake ni kuudhibiti kikamilifu mfumo wa kidini wa Mashia na kuondoa uwezo wowote wa kujisimamia kwa kujitegemea.

Mamlaka ambayo inadai kutetea kuishi pamoja inawachukulia Mashia si kama wananchi wenza wenye usawa, bali kama tatizo la kiusalama ambalo lazima lidhibitiwe kila wakati.

Kwa hiyo, kila jambo linalohusiana na utambulisho wao huangaliwa kwa mashaka: wanazuoni, Husainiyya, ibada na alama za dini, wahubiri, wakfu, na hata matukio ya kidini ambayo Bahrain imeyashuhudia kwa miongo mingi bila kuwa tishio kwa yeyote.

Ni nini kinachofuata?

Baadhi wanaamini kwamba serikali itaongeza kiwango cha mvutano dhidi ya dhehebu hili na haitatosheka na maamuzi yaliyotangulia.

Hali ya hatari zaidi ni kulenga maadhimisho yajayo ya Ashura.

Si tu kwamba huenda tukashuhudia kuzingirwa kwa misafara na Husainiyya kubwa au hata ndogo, bali serikali inaweza kujaribu kuondoa sura ya Ashura ambayo Mashia huiwasilisha kila mwaka katika ramani ya matukio ya nchi za Kiislamu.

Kwa sababu Mashia wa Bahrain wamekuwa wakijitofautisha katika kuhuisha kwa mpangilio mkubwa maombolezo ya Kihussein, zikiwemo shughuli za mitaani, misafara, majlisi nyingi za maombolezo, pamoja na utofauti na wingi wa kazi za kisanii na kishairi zinazotolewa kila mwaka.

Taswira hii sasa imekuwa jambo linaloisumbua serikali ambayo imeanza kuchoshwa nayo.

Badala ya kurahisisha zaidi shughuli hizi, au angalau kunufaika nazo, hofu ya kuongezeka kwa hatua za kuingilia kati kupitia kubana zaidi kutoka kwa maandamano ya maombolezo ya Kihussein (kama ilivyozoeleka katika njia zinazojulikana nje ya Husainiyya) na kukandamiza uhuishaji mkubwa wa wananchi inaongezeka.

Kwa hiyo, leo swali si tena ikiwa kuna vita dhidi ya uwepo wa Mashia nchini Bahrain au la, bali ni kwamba; mamlaka tawala zinaweza kwenda mbali kiasi gani katika njia hii ambayo iko wazi kuelekea kuongezeka zaidi kwa mvutano.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha